Harmonize: Huwezi kushinda Grammy kwa kusalimia watu

Harmonize: Huwezi kushinda Grammy kwa kusalimia watu

Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini Harmonize amerusha dongo kwa msanii mwenzake Diamond baada ya kushindwa kuchaguliwa kuwania tuzo za muziki Marekani Grammy kwa kudai kuwa huwezi kuchaguliwa katika tuzo hizo kwa kusalimia watu.

Harmonize ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye mahojiani na waandishi wa habari usiku wa kuamkia leo Novemba 23,2024 kwa kueleza kuwa ili kuchaguliwa katika tuzo hizo inabidi kazi zako zionekane na sio kushinda kwa kusalimia watu.

“If you talk about Grammy unazungumza Grammy winer 2025 we can not win Grammy just for greet people harafu msichokijua hata Grammy hawajui kama ni maarufu hawajui kama unajulikana so let focus kwenye music “, amesema Harmonize


Mbali na hayo pia ameweka wazi kuwa mwaka 2025/2026 atachaguliwa na atashinda tuzo hiyo.

Utakumbuka kuwa baada ya Diamond kushindwa kuchaguliwa katika tuzo hizo alifunguka kwa mara ya kwanza na akieleza kuwa bado hajakata tamaa anamiini ipo siku atashinda tuzo hizo.


“Kuna watu wengi kwa bahati mbaya pia hawakuchaguliwa na wamefanya vizuri sana kwa sisi tuamini kwamba tumefanya kazi bora tumepata mwanzo mzuri wa kuifungua dunia sasahivi ni kumwaga mawe mengi Mungu pengine katuandikia mwakani. Labda hatuingii tu kwenye kategori tutaondoka na 10 pale mimi naamini sana kwenye kila kitu kinawezekana, sasa inapotokea kitu umekikosa sio uanze kuchanganyikiwa na maneno ya watu huko mtandaoni hapana jenga tena mkakati wako”, amemalizia Diamond


Octoba,2024 Diamond aliwasilisha wimbo wa ‘Komasava’ uliotazamwa zaidi ya mara milioni 29 kwenye mtandao wa YouTube. Lakini mambo yamekuwa magumu upande wake kwa jina lake kutotajwa kuwania tuzo hizo katika vipengele alivyoorodhesha.

Diamond aliwasilisha jina lake kupitia wimbo wa 'Komasava' katika vipengele viwili, kwanza Video Bora (Komasava) na Mtumbuizaji Bora kutoka Afrika.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags