Harmonize aeleza ukaribu wake na Tanasha
Baada ya mwanamuziki kutoka Kenya na mzazi mwenzie na msanii Diamond, Tanasha Donna kukoment utani kwenye moja ya video ya Harmonize, hatimaye Konde amefunguka ukaribu wake na Tanasha huku akidai kuwa hawana ukaribu wowote na mwanadada huyo.
Konde ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye mahojiano na waandishi wa habari usiku wa kuamkia leo Desemba 6, 2024 katika uzinduzi wa album ya msanii wake Ibraah ambapo alieleza kuwa anamjua msanii huyo lakini hawana ukaribu wowote.
“Hamna Tanasha sina ukaribu nae wowote kihivyo ananifollow nami namfollow nimepost amekoment for respect na mimi nilimjibu tu lakini she’s good musician ikitokea tukipata nafasi ya kufanya wimbo ni sawa tuu, sisi hatuna kitu chochote na wala hatujawahi kuonana tukazungumza,” amesema Konde Boy
Utakumbuka kuwa siku moja iliyopita kupitia ukurasa wa Instagram wa Konde alishare video akiwa na Malaika ambapo Tanasha aliingia upande wa komenti na kumbatiza jina Harmo kwa kumuita ‘Mr Nyash’.
Leave a Reply