Hali ya biashara za furniture mwisho wa mwaka

Hali ya biashara za furniture mwisho wa mwaka

Hey hey! watu wangu wa nguvu, mwaka ndiyo huo unatuaga na leo kwenye biashara tupo na jambo ambalo familia nyingi ni ngumu kulifanya mpaka pale watakapoona kitu kimevunjika au kuharibika.

Tumezoea kuona baadhi ya familia kubadilisha furniture kwenye majumba yao kila ifikapo mwisho wa mwaka lakini kuna wale wenzetu na siye ambao hatubadilishi mpaka kiharibike.

Mfano mkubwa miswaki, kuna baadhi ya watu mwaka wa pili huu sasa unaenda kuisha au mwaka mmoja hajabadilisha mswaki mpaka utakapo dondoka chooni au uvunjike.

Wiki hii tunakusogezea biashara ya furniture kuelekea mwisho wa mwaka Mwananchi Scoop tukakutana na muuzaji wa thamani za ndani aitwaye Zack Furniture kutoka Kigamboni jijini Dar es salaam amefunguka mengi kuhusiana na biashara kipindi hichi cha mwisho wa mwaka kwa kueleza…

“Biashara kwa upande wangu mimi naona kila siku ni nzuri na hii inatokana na mitindo mipya inayoendelea kutoka kila siku so mimi naona biashara iko vizuri kila siku” amesema Zack

Na kuhusu watu kubadilisha vitu vya ndani mwisho wa mwaka alifunguka na kueleza kuwa baadhi ya watu hawana desturi hiyo mpaka pale watakapoona kitu hicho kimeharibika, huku akisisitiza kuwa watu wengi siku hizi wanabadilisha vitu vyao kutokana na kuvutiwa na mitindo mipya ya furniture .

Aidha hatukuishia hapo tukapita mitaa hiyo na kuuliza baadhi ya wakazi kuhusiana na kubadilisha furniture ndani ya nyumba kila mwisho wa mwaka walieleza kuwa hawana desturi hiyo mpaka pale kimoja kitakapo haribika huku wakisema kuwa hali ngumu ya maisha ndiyo inachangia yote hayo.

Kama mnavyojua Mwananchi Scoop hatunaga jambo dogo moja kwa moja tukamvutia waya mwanamama Mwanahanuni Mohammed mkazi wa Mbagala Chamazi yeye alieleza kuwa huwa anabadilisha vitu vyake vya ndani kila mwaka.

“Mimi huwa nina desturi ya kubadirisha furniture za ndani kila ifikapo mwisho wa mwaka na hapa zimepita wiki kadhaa tuu tangu nibadirishe vitu vyangu vya ndani” amesema Mwanahanuni

Mwanahanuni anasema huwa anabadirisha furniture za ndani ili aweze kuendana na mitindo mipya kwa sababu furaha yake ni kuona nyumba yake inapendeza na iko tofauti kila mwaka, na hii inatokana na kuzoeshwa na wazazi wake kubadilisha vitu vya ndani kila mwaka.

Baada ya kujua sababu pia tulimuuliza swali mwanamama huyo kuhusiana na wakati anabadirisha vitu vipya vya zamani huwa anavipeleka wapi alisemaaa..

“Mimi huwa nafanya top up kama watu wanavyofanya kwenye simu za I phone siku hizi, huwa napeleka vitu vya zamani kwa mafundi vikaboreshwe na kutengenezwa kama mimi ninavyotaka na ambavyo siyo vya kufanya hivyo huwa naviuza na kuongeza pesa ili niweze kununua vitu vingine” amesema Mwanahanuni

Haya haya! wasomaji wetu wa Scoop naona tunaendelea kuelewana taratibu kuwa kuna baadhi ya familia wanaamua kubadili mtindo ya maisha yao na kuishi, maisha ambayo wanaishi wenzetu wa nje na siyo kama wanatumia pesa kubwa kufanya hivyo hapana ni maamuzi  hata wewe ukiamua unaweza.

Tukutane next yeahhhhhhhh, na asanteni sana kuwa pamoja nasi kwa mwaka huu wote, msiache kufuatilia jarida letu la @Mwananchiscoop maana kuna suprise kibao tumewaandalia.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags