Guinness yathibitisha Hilda kuvunja rekodi ya dunia ya mpishi

Guinness yathibitisha Hilda kuvunja rekodi ya dunia ya mpishi

Mpishi kutoka nchini Nigeria ambaye amekuwa maarufu duniani kote baada ya kupika bila kukoma kwa zaidi ya saa 93 amethibitishwa kuwa mshikilizi mpya wa rekodi ya dunia.

Shirika hilo baada ya kupitia video zote za siku 4 ambapo mpishi huyo alikuwa katika mashindano, sasa wameweka wazi na kuthibitisha kuwa amevunja rekodi ya kupika masaa mengi.

Wanasiasa na watu mashuhuri walimshangilia Hilda Baci jikoni kwake huko Lagos wakati wa kipindi cha siku nne mwezi uliopita.

Alitumia zaidi ya sahani 100 katika mchakato huo na aliruhusiwa tu kuchukua mapumziko ya dakika tano kila saa. Baci amemshinda mshikilizi wa zamani wa rekodi Lata Tondon wa India, ambaye alisimamia muda wa saa 87 dakika 45 mwaka wa 2019.

The Guinness Book of World Records, ambao walilitoa uamuzi wa shindano la kupikia za Baci, wameshare video kupitia mitandao yao ya kijamii wakimpongeza kwa kuweka rekodi.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags