Guinea ya ikweta yapiga marufuku hukumu ya kifo

Guinea ya ikweta yapiga marufuku hukumu ya kifo

Guinea ya Ikweta Afrika ya kati imepiga marufuku hukumu ya kifo na taarifa hiyo imetolewa kupitia televisheni ya taifa hilo ambapo ilitangazwa jana Jumatatu kwamba hukumu ya kifo imepigwa marufuku kabisa baada ya rais wa Guinea ya Ikweta,Umaro Sissoco Embaló kutia saini sheria mpya.

Makamu wa rais wa nchi hiyo Teodoro Nguema Obiang Mangue ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kuthibitisha sheria hiyo.

Sheria hiyo mpya itaanza kutekelezwa katika kipindi cha siku 90 baada ya kuchapishwa katika gazeti rasmi la serikali na baada ya kuridhiwa na bunge.

Aidha Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International, hukumu ya kifo ilitekelezwa rasmi mara ya mwisho nchini Guinea ya Ikweta mnamo 2014.

Aloooooh! Haya mdau na mfuatiliaji wa Mwananchi Scoop ni sheria gani ungependa ipigwe marufuku dondosha komenti yako hapo chini.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags