Guchi apanga kuvujisha nyimbo aishutumu lebo yake

Guchi apanga kuvujisha nyimbo aishutumu lebo yake

Mwanamuziki wa Afropop kutoka nchini Nigeria, Guchi ameelezea kutoridhishwa kwake na lebo yake ya PG Records Entertainment kwa kuchelewesha kuachia wimbo aupendao.

Guchi ana amini kuwa muziki ni zawadi ya bure kutoka kwa Mungu na anataka shauku yake iheshimiwe na kutoa onyo kuwa ikiwa hautatoka atavujisha yeye mwenyewe.

Hitmaker wa Jennifer ameendelea kusisitiza kuwa muziki haupaswi kuwa jambo lenye ugumu kiasi hicho.

“Una andaa wimbo kwa moyo wote, unakutana na sababu nyingi ambazo zinakuzuia kutoa wimbo huo, kwanini taratibu nyingi zinahitajika katika jambo ambalo ni zawadi ya bure kutoka kwa Mungu?”alisema Guchi.

Ikumbuke sio tu huyo ambaye amekumbana na changamoto hiyo ila wasanii kama Azealia Banks, Lauryn Hill, Kanye West na wengine waliwahi kuzishutumu lebo zao kwa taratibu mbovu na kutaja ucheleweshaji huo kuwa kikwazo kikubwa katika kukamilisha na kuziachia kazi zao.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags