Geay aibuka mshindi mbio za B.A.A

Geay aibuka mshindi mbio za B.A.A

Mkimbiaji mahiri wa mbio ndefu nchini Tanzania, Gabriel Geay aliibuka mshindi katika mbio za 10K, 2023 za Chama cha Wanaume cha Boston (B.A.A.) jana Jumapili, akimaliza kozi kwa saa 27:49.

Geay, ambae ni bingwa wa 2018, aliwashinda wanariadha wawili wa Kenya, Edwin Kurgat (28:01) na Alex Masai (28:09), na kutwaa taji hilo.

Waliomaliza watano bora katika kinyang'anyiro cha wanaume walikuwa Tsegay Kidanu kutoka Ethiopia, aliyemaliza kwa muda wa 28:18, na Diego Estrada kutoka Mexico, aliyemaliza kwa muda wa 28:19.

“Nilijaribu kusukuma mwanzoni, na kutoka 6K au 5K na kuendelea, nilijaribu tena kuisukuma. Kulikuwa na watu watatu nyuma yangu, lakini katika mita chache walishuka. Nilikuwa na nia ya kushinda,” alisema Geay,  ambaye anatoka katika nafasi ya pili katika mbio za Boston Marathon mwezi Aprili.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags