Gachagua: hatutazungumza na Odinga hadi amtambue Ruto kuwa ni rais

Gachagua: hatutazungumza na Odinga hadi amtambue Ruto kuwa ni rais

Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua, ametoa masharti kwa Kiongozi wa Azimio La Umoja Kenya, Raila Odinga  na kusisitiza anatakiwa akiri hadharani kuwa anamtambua William Ruto  kuwa ndiye Rais wa nchi hiyo.

Gachagua amesema kuwa “Unazungumzaje na mtu ambaye hatambui utawala wako? Yeye ni nani hapa Kenya? Ni raia wa kawaida lakini kama ana mahitaji yake binafsi aje tuzungumze, hajachaguliwa na mtu yeyote." Amesema Rigathi

Odinga alitangaza kusitisha maandamano ya kupinga gharama za maisha kupanda yaliyoanza wiki mbili zilizopita ili kuzungumza na Serikali ya Ruto, lakini ametishia kurejesha maandamano hayo ikiwa hakutakuwa na mazungumzo kati yake na Serikali






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags