Fulham wagoma kumuachia Aleksandar Mitrovic

Fulham wagoma kumuachia Aleksandar Mitrovic

Baada ya kuthibitika kuwa #FulhamFC imezuia uhamisho wa mshambuliaji wa timu hiyo #AleksandarMitrovic, kwenda 'klabu' ya Al Hilal ya Saudi Arabia, mshambuliaji wa huyo ameripotiwa kukataa kuichezea tena 'timu' hiyo.

FulhamFC walikataa ofa mbili kutoka kwa #Al Hilal kwa ajili ya kumchukua Mitrovic, ikiwemo ofa ya pauni milioni 35 iliyokataliwa 'wiki' iliyopita, kwa madai ya kuwa mshambuliaji huyo aliyepachika mabao 15 katika michuano yote msimu uliopita anathamani ya Pauni milioni 52.

Jambo hilo lilimkasirisha Mitrovic, na kuamua kuwataarifu ndugu zake hatoichezea 'klabu' hiyo tena.

Awali iliripotiwa kuwa Mitrovic hakutaka kurejea kikosini kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao, lakini baada ya mazungumzo, Fulham wamefanikiwa kumshawishi kurejea kikosini.

Mitrovich ataungana na wachezaji wengine kuelekea nchini Marekani kwa ajili ya maandalizi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags