Forbes yaitaja Tz kama sehemu ya kutembelea 2022

Forbes yaitaja Tz kama sehemu ya kutembelea 2022

Moja ya story inayobamba mitandaoni ni ya Tanzania kutajwa kuwa ni miongoni mwa maeneo salama na mazuri kutembelea duniani kwa mwaka 2022.

Hii ni kwa mujibu wa maoni yaliyokusanywa na Jarida la Forbes juu ya maeneo gani bora ya watu kwenda kufurahi na kupumzika haswa baada ya hali kuanza kuwa shwari baada ya janga la Uviko-19.

Tanzania imependezwa na Alyssa Ramos,  mtayarishaji maudhui na mjasiriamali ambaye ameyataja maeneo mengi ikiwemo Zanzibar, Hifadhi ya Ruaha, Serengeti na maeneo mengine.

Naimani na wewe utaungana na jarida hili kuwa Tanzania ni sehemu salama kabisa kutembelea hivyo ni wajibu wetu kama watanzania kutembelea mbuga za wanyama na maeneo mengine ya utalii.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags