Filamu Ya MJ Kutoka Oktoba 2025

Filamu Ya MJ Kutoka Oktoba 2025

Filamu inayoonesha na kuelezea maisha halisi ya mfalme wa Pop Duniani Michael Jackson ‘MJ’, imepangwa kuoneshwa rasmi kwa mara ya kwanza Oktoba 3, 2024 baada ya kuhairishwa tarehe iliyotangazwa hapo awali ambayo ni April 18, 2025.

Kwa mujibu wa Billboard imeeleza kuwa sababu ya kusogezwa mbele ni kutokana na changamoto zilizoikumba timu ya waandaji kwani walipanga kuanza kurekodi filamu hiyo mwaka 2023 lakini kutokana na changamoto hizo walianza kurekodi Januari 2024.

Jaafar Jackson ambaye ni mpwa wa Michael Jackson, ndio ataigiza kama muhusika mkuu, huku Nia Long, Laura Harrier, Miles Teller, na Colman Domingo wakishiriki nakukamilisha orodha ya waigizaji katika filamu hiyo.

Jaafar mwenye umri wa miaka 25 ni mwanamuziki na dansa ambaye alianza kuimba rasmi akiwa na umri wa miaka 12, na alianza kujulikana zaidi mwaka 2019 baada ya kuachia wimbo wake wa ‘Got Me Singing’.

Ikumbukwe kuwa Michael Jackson alizaliwa mwaka 1958 na kufariki dunia mwaka 2009. Alitamba na nyimbo zake kama Smooth Criminal, Thriller, Will You Be There na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags