Fanya mazoezi haya kukuza kifua bila vifaa vya uzito

Fanya mazoezi haya kukuza kifua bila vifaa vya uzito

Habari kijana wenzangu natumaini u mzima wa afya na unaendelea na majukumu yako ya hapa na pale ya kusoma au kujiingizia kipato kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.

Hata hivyo leo kwenye dondoo ya masuala ya Diet na Fitness tunakuletea aina ya mazoezi ya kukuza kifua bila kutumia vifaa vya uzito.

Watu wengi wamekua wakijiuliza ni namna gani mtu anaweza kujenga misuli ya kifua bila ya kubeba vitu vizito, basi leo tutagusia swala hilo na natumae litawasaidia.

Tunapaswa kwanza kuelewa kuwa kifua kimejengwa na misuli iitwayo pectoralis major ambayo ipo karibu na torso (munganiko wa mabega na mikono). 

Zifuatazo ni njia ya kukuza misuli hiyo ya kifua kwa kutumia mwili pekee, ambazo ni;

Pushups za kawaida

Pushups za kawaida uhitaji mtu kusukuma mwili kutoka chini na kuiweka nyuzi tisini (90), ambapo itakuhitaji ufanye marudio kulingana na idadi utakayo pendelea kufanya. Hili zoezi husaidia kukaza misuli ya kifua na pia kutengeneza muonekano mzuri wa kifua.

Pushups za inklin 

Hii ni aina ya pushup inayo muhitaji mtu aweke mikono pahali pajuu palipo inuka kidogo kutoka chini kama mita moja nakuweka mikono nyuzi tisini (90) kutoka pahali ulipoweka viganya vya mikono.

Zoezi hili lina kulazimisha kujinyanyua juu na chini, kwa mizunguko kadha kwa idadi unazozitaka...Hili zoezi usaidia kukaza misuli ya mikono na pia kutengeneza kifua cha chini.

Pushups za muinuko

Hii ni aina ya pushup inayo muhitaji mtu aweke mikono pahali palipo shuka kutoka sehemu ulipo weka miguu. Hapo inampasa mtu aweke mikono chini ikiwa imekaa usawa wamabega na nyuzi tisini (90) kutoka chini.

Zoezi hili lina kulazimisha kujinyanyua juu na chini, kwa mizunguko kadha kwa idadi unazozitaka.

Zoezi la kujivuta juu

Hili zoezi humuhitaji mtu kujishikilia pahali pa juu palipo inuka ambapo miguu haigusi chini kirahisi, na kujishkiza mikono kwenye sehemu kama vile (chuma).

Umuhimu wa zoezi hili ni kwamba husaidia kuvuta kifua cha juu( chini ya kidevu) na hivyo kuweka muonekano mzuri wa kifua.

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post