Familia za watoto walifariki nchini Gambia kutokana na dawa za kikohozi zakataa fidia

Familia za watoto walifariki nchini Gambia kutokana na dawa za kikohozi zakataa fidia

Familia za watoto 70 waliofariki kutokana na majeraha ya figo yaliyohusishwa na dawa za kutibu kikohozi zilizotengenezwa nchini India, zimekataa ofa ya fidia ya jumla ya Dola za Marekani 20,000 (Takriban Tsh. Milioni 46 za kitanzania) kwa familia zote kutoka kwa Serikali ya nchi hiyo.

Familia hizo zimesema kukubali fedha hizo kunatafsirika kuwa hawapiganii haki hivyo zinataka Shirika la Serikali la Kudhibiti Dawa kuondoa madai yake ya awali, kwamba watoto hao walifariki kwenye maji ya mafuriko na si kutokana na dawa hatari.

Aidha wanataka Shirika hilo kuondolewa katika uchunguzi wa sakata hilo, ulioagizwa na Rais.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags