Fainali kombe la dunia 2026, Kufanyikia New Jersey

Fainali kombe la dunia 2026, Kufanyikia New Jersey

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limetangaza kuwa fainali ya Kombe la Dunia la 2026 itafanyika kwenye Uwanja wa #MetLife  unaochukua mashabiki 82,500 katika mji wa East Rutherford, kisiwani #NewJersey  Julai 19, 2026.

Inaelezwa kuwa ratiba ya mashindano hayo iliyozinduliwa siku ya jana Jumapili imebainisha kuwa  yatashirikisha  Mataifa 48 na kufanyika katika miji 16 kutoka Marekani, Canada na Mexico.

FIFA imetaja viwanja vitatu vitakavyotumika kwenye ‘mechi’ za waandaaji wa fainali hizo ambao ni Mexico, Canada na Marekani ambapo Mexico itaanzia Estadio Azteca huko Mexico City Juni 11, Marekani itaanzia Los Angeles Juni 12 huku Canada ikianzia Toronto Juni 12.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags