Faida za kula utumbo kwa binadamu

Faida za kula utumbo kwa binadamu

Nyama ya matumbo au utumbo ni kipande cha nyama inayotoka katika tumbo la wanyama kama vile ng'ombe, nguruwe, kondoo na mbuzi.

Nyama hii inaweza kupatikana katika mikahawa barani Asia, Afrika, baadhi ya maeneo ya Amerika na bara Ulaya. Nyama hii ina faida nyingi katika mwili wa binadamu ikilinganishwa na nyama nyingine.

Upande wa kiafya, nyama ya matumbo au utumbo ina manufaa mengi ikiwemo wingi wa protini na virutubisho vingine ambavyo ni muhimu kwa afya ya binadamu.

Faida za kula nyama ya utumbo

Utumbo una vitamini na madini mengine ambayo ni muhimu kwa mwili wa binadamu na unapoliwa una virutubishi ambavyo vina faida kwa afya zetu, kulingana na mchambuzi wa afya wa Webmd.com.

  1. Inazuia upungufu wa damu mwilini

Utumbo una vitamini B12, ambayo huzuia upungufu wa damu mwilini, hususan miongoni mwa watu waliochoka na wasioweza kutembea.

  1. Inajenga mifupa na misuli mwilini

Nyama ya utumbo ina protini inayosaidia kujenga misuli na mifupa. Vilevile nyama hiyo ina asidi zote 9 muhimu ambazo mwili wetu unahitaji kufanya kazi, kulingana na Healthline.com.

  1. Imejaa madini na vitamini

Nyama ya utumbo ina virutubisho kama vile madini ya zinki, selenium na kalsiamu. Zinki husaidia watu seli za mfumo wa kinga wa mwili kusaga vyakula vya wanga. Selenium husaidia kuboresha jeni na afya.

 

 

  1. Kupunguza uzani/ uzito wa mwili

Kula vyakula vyenye protini nyingi husaidia kudhibiti lishe na kupunguza uzito. Utumbo una viwango vya chini vya Kalori ikilinganishwa na vyakula vingine.

Ulaji wa vyakula vyenye protini nyingi humsaidia mtu kupunguza uzito na kupunguza kiwango cha ulaji wa chakula, kwa mujibu wa Healthline.com.

  1. Hatari ya kuvimbiwa/ tumbo kujaa/ kushiba kupita kiasi

Nyama ya utumbo ina mafuta mengi ikilinganishwa na nyama nyingine na watu walio na mafuta mengi mwilini wanaweza kuathiriwa kwa njia tofauti.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags