Wanawake oyeeeeeh! Kaulimbiu yetu ni ile ile bila hata ya kuwezeshwa wenyewe tunaweza, haki sawa kwa wote, kama tunavyojua wiki hii ilikuwa ni maadhimisho ya siku ya wanawake duniani. I hope kila mmoja aliifurahia siku hiyo.
Kama kawaida yetu biashara ndo kila kitu kwetu, sasa leo tumekuja na jambo la muhimu sana katika maisha, sio kwenye biashara tu. Kupanga bajeti, biashara yako ili iendelee na ikue lazima upange bajeti na hii itakusaidia kuiona faida ya unachokifanya.
Faida na umuhimu wa kupanga bajeti ya biashara yako, pamoja na manufaa ya kupanga bajeti kwenye maisha ya kila siku kwa ujumla.
- Utaweza kujua fedha zako mahali zinapokwenda
Ukiwa hauna bajeti na unaingiza kipato kila siku au kila mwezi unaweza ukawa unapata pesa nzuri sana lakini ukawa huelewi fedha zinaenda wapi au umezifanyia kazi gani, kwani utajikuta unafanya manunuzi ya vitu ambavyo sio mahitaji yako muhimu.
Bajeti itatenga kila fedha unayoipata ifanye kazi gani au uifanyie manunuzi gani na sio unakurupuka kununua nunua vitu bila kuwa na mpangilio, lakini pia utapata kuelewa mahitaji yako kwa siku ni kiasi gani na kukupa motisha ya kuongeza kipato chako.
- Itakuepusha na hatari ya kufilisika
Ukiwa na tabia ya kuweka bajeti ya matumizi ya pesa kila siku moja ya jambo utakaloepuka nalo ni pamoja na kuepuka kufilisika kwani unapoifuata bajeti unaepuka kutumia pesa zaidi ya ile unayoipata.
Kuna baadhi ya watu ambao wanafanyabiashara ya kuuza duka au genge, kwao ni rahisi kufilisika kwasababu baadhi yao ,matumizi ya nyumbani wanategemea hapo hapo dukani, so epuka sana kufanya jambo hili maana utafilisika mchana kweupeee.
- Husaidia kuepukana na madeni
Ukiwa na bajeti itakusaidia kununua vitu kwa cash na pia ukiwa na bajeti pesa yako unaouwezo wa kuweka akiba ya kipato unachokipata kila siku. Na madeni yanakuja pale unapotumia pesa za bidhaa uliouza au pesa ya ofisi, so epuka madeni madogo madogo ndo maana watu wengi hawapendi wao ndo wakae kwenye biashara zao, maana wanajua lazima watumie kile wanachokipata.
- Husaidia kuepuka na matumizi makubwa ya pesa
Bajeti hukupatia mwongozo wa kufuata kipi ununue na kipi usinunue kwa wakati huo kwani kiasi kilichopangwa kwa siku, wiki au mwezi ndicho kitakacho kukuruhusu au kutokuruhusu kufanya manunuzi.
Ukishamaliza kupanga bajeti za bidhaa zako basi inabidi upange na vile vitu ambavyo una uhakika navyo vitakuwa vya umuhimu kila siku mfano, chakula nk. Unapofanya bajeti zako hili ni swala la muhimu sana ili uepukane na matumizi makubwa ya pesa, basi ukiweza kufanya hivi utaifurahikia biashara yako na jambo unalo lifanya.
- Inasaidia kutimiza malengo ya muda mrefu
Kama tunavyojua kila kitu ni malengo hata yule anayesoma ana malengo yake na mfanyabiashara vivyo hivyo, Bajeti kama mwongozo wa matumizi ya pesa au kipato chako, itakusaidia sana pale ukiwa na malengo ya nunua au kuanzisha kitu fulani kikubwa.
Kupanga bajeti kwa makini na kutoingilia kati bajeti yako kutakusaidia sana kufikia malengo yako yale ulioyapanga yatatimia bila shaka.
Ooooooh! I hope wote tumeelewana so anza sasa kupanga bajeti ili ufurahie unachokifanya. Waswahili wanasema mali bila daftari huisha bila habari, daftari litakusaidia sana kwenye kupanga bajeti zako, hasa ukiwa biashara unamuachia mtu ukiwa unafuatilia kwa kupanga bajeti utaweza kujua kuwa huyo mtu anakuibia au laah!
Leave a Reply