Faida, hasara za biashara ya nguo za mitumba

Faida, hasara za biashara ya nguo za mitumba

Nguo za mtumba ni nguo ambazo zimekuwa kizipendwa na kuvaliwa na watu wengi kutokana na utofauti wake, yaani ni nadra sana kukuta nguo hizo zilizofanana.

Huku sababu nyingine ya kuzipnda ikiwa ni bei rahisi yaani kila mtanzania anauwezo wa kuinunua.
Mwananchi Scoop imefanya mahojiano na mmoja wa wauzaji wa nguo za mtumba aitwaye Rehema Suleiman anayepatikana Kigamboni Ferri jijini Dar es Salaam.

Rehema ni mfanyabiashara na mwanafunzi wa Mwaka wa pili katika chuo cha CBE ambaye anajishughulisha na biashara ya nguo za mitumba.

Kupitia mahojiano hayo Rehema amefunguka mengi kuhusia na biashara hiyo, changamoto, faida, hasara pamoja na soko likoje kwa kueleza,

“Kwa sasa soko ni zuri kabisa kwani tumekuwa tukipata faida kubwa na hii ni baada ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali kuanza kuvaa nguo za mtumba na siyo kama zamani wanafunzi wengi walikuwa wakivaa nguo za dukani” amesema Rehema

Aidha aliendelea kwa kueleza changamoto na hasara anazokumbana nazo katika biashara hiyo ambapo aliweka wazi kuwa changamoto kubwa na ambayo haiepukiki ni kukuta nguo nyingi zimechaniki au zisizofaa katika mabalo ya nguo wanayonunua.

“Changamoto ambayo inaturudisha nyuma ni kukuta baadhi ya nguo zikiwa zimechanika na sometime unaweza kukuta karibu nusu ya balo unalonunua lakini ndiyo hivyo hatuwezi kukata tamaa kutokana na ndiyo biashara tuliyoichagua” amesema Rehema

Hata hivyo aliweka wazi kuwa ukinunua balo la mtumba grade one linaweza kukupatia faida mara mbili ya unayo nunua.

“Hii biashara inafaida kubwa sana pale utakapoiwekea maanani na kuwa nayo serious kwani mimi huwa Napata mara mbili ya pesa ninayonunulia balo la mtumba, na huwa na nunua balo moja kuanzia laki tatu hadi laki tano nikija kuuza hapo naweza kupata hadi milioni moja, ifike mahali baadhi ya watu waache kuidharau biashara hii kwani ndiyo inayotufanya wengine tuendelee kutamba mjini” amesema Rehema

Aidha mwanaunzi huyo anayejishughulisha na biashara pia alitoa ushauri kwa wanafunzi wenzake pamoja na vijana waliopo mtaani akiwataka waache kujibweteka na kusubiri kuajiliwa kwani zipo biashara ambazo wanauwezo wa kuzifanya na zikawafanikishia maisha yao.

Ameeleza kuwa siyo lazima mtu kuuza nguo za mtumba kama yeye, unaweza kuangalia kitu ambacho mtaani kwako hakuna na ukakifanya kama fursa ya kujipatia kipato.


Aidha hatukuishia hapo tukakutana na kijana ambaye pia anajishughulisha na biashara hiyo ya uuzaji wa nguo za mitumba aitwaye Abdallah sule maarufu Dubai mkazi wa Dar es Salaam ameeleza chanagmoto anazokumbana nazo katika biashara hiyo.

“Biashara ya nguo za mtumba ni biashara yenye faida sana, pia ina changamoto nyingi moja kati ya hizo ni kukuta nguo chache nzuri wakati wa kufungua balo lako jambo ambalo linapelekea sisi kama wafanyabiashara kupata hasara, changamoto nyingine ni biashara kuwa ngumu kwenye baadhi ya miezi haswa wa kwanza” amesema Dubai.

Aidha aliongezea kwa kueleza kuwa kwa upande wake anaiona ni biashara nzuri wanayoweza kufanya vijana na ikawapatia kipato, lakini jambo la kuzingatia zaidi ni sehemu anayokwenda kununulia balo lake kutokana na kuwa na matapeli kila kona.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags