Fahamu njia za kufanikiwa kimaisha ukiwa chuoni

Fahamu njia za kufanikiwa kimaisha ukiwa chuoni

Leo katika Karia tunazo funguo za kukusaidia wewe Mwanachuo kupata maarifa watakayokufanya ufanikiwe kimaisha pindi bado upo chuoni.

Nikuweke wazi tu kwamba unaweza kufanikiwa Kimaisha kuanzia Chuoni, hata kama umechaguliwa kwenye chuo usichokipenda au kozi unayoisoma umeambiwa haina soko.

Haijalishi uko mwaka wa kwaanza, wa Pili, wa Tatu, wa Nne, au wa Tano, kama ukifuata njia hizi hapa chini basi lazima utatoboa tu kimaisha kijana mwenzangu.

  1. Weka akiba

Kiukweli ukiwa chuo ndio muda mzuri wa kujifunza kuweka akiba, muda mzuri wa kujifunza kuwa na matumizi mazuri ya hela. Hasa kama unapata boom au una biashara unayoifanya inayokuingizia pesa, usitumie hela vibaya chuoni.

Weka akiba kwani fedha hiyo inaweza kukusaidia hata ukimaliza chuo zikawa nauli za kwenda kwenye interviews.

  1. Kutengeneza mahusiano mazuri na watu

Njia hii ya kutengeneza mahusiano mazuri na watu hasa wanafunzi wenzako ni muhimu sana pindi unapokuwa chuoni maana ufahamu atakayekuja kukusaidia mbeleni.

 

Jamani kuna maisha baada ya chuo. Kuna wale watakaoshare fursa na wewe, watakaokusupport utakayoyafanya baada ya chuo na wale watakao kuwa nawe kwenye maisha baada ya chuo.

Tengeneza mahusiano mazuri na watu, sio wote maana usije ukawa unajipendekeza tu ila hakikisha una watu wanaokuthamini na unaowathamini, na pia usipopata watu wa hivyo chuoni hakuna shida pia.

  1. Soma vitabu

Ili kuweza kujiongezea maarifa mengi zaidi huna budi kusoma vitabu tofauti na vile unavyosoma darasani.

Hakika unapata muda wa kusoma vitabu vya topic mbalimbali tofauti na vya chuo ili ujifunze kuhusu maisha ya watu wengine waliofanikiwa.

  1. Kujitambua (kujitafuta)

Muda huu ambao uko peke yako, unaingia kwenye utu uzima, ni vizuri kuutumia kujitafuta, kujifunza kuhusu wewe, kujitambua, misimamo yako, nini unapenda, njia gani unapenda kuishi maisha yako usiwe tu mfuataji wa trends.

Nafahamu kuwa vijana wengi chuoni tunapenda kufatilia maisha yaw engine na kushindwa kujitambua sisi wenyewe tunataka kufanya nini na kwa wakati gani.

Badilika sasa anza kujitambua na kuwa na misimamo yako katika kila jambo la manufaa ambalo utalifanya.

  1. Anza kufikiria project utakazozifanya

Ukiwa chuoni usikae kizembe anza kufikiria project mbalimbali utakazozifanya pindi tu utakapomaliza chuo.

Ni vizuri sana kuanza kufikiria project unayotamani kuifanya ukiwa chuoni mapema, kuliko kukurupuka kuchagua wakati muda umefika wa kupresent.

  1. Kujiandaa na maisha ya mtaani

Jiandae na maisha ya mtaani, ndio unapaswa kujiandaa na hilo maana ni lazima umalize masomo na urudi mtaani.

Hakikisha unafikiria kuhusu maisha yako baada ya chuo, wengi tunawaza utapata kazi, ila kaa chini fikiria mambo yote, vipi kama usipopata? Vipi kama ukichukua muda kupata kazi? Utaishi wapi? Umetengeneza CV yako.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags