Fahamu kuhusu vidonda vya tumbo

Fahamu kuhusu vidonda vya tumbo

Na Mark Lewis

Vidonda vya tumbo (Peptic Ulcers) ni tatizo linalotokea baada ya kuta za tumbo au utumbo mdogo kuwa na vidonda. Hii hutokea baada ya kuharibika kwa ukuta wenye ute unaozuia kemikali za kuyeyusha chakula unaoitwa ‘mucus’. Kemikali ambayo ni asidi inayozalishwa mwilini kiasili husaidia kuyeyusha chakula na kuua wadudu tumboni, kama vile ukuta wenye ute ukiharibiwa na kushindwa kufanya kazi basi kemikali (acid) itaathiri tumbo au utumbo na kuruhusu bakteria kuendelea kusababisha vidonda vya tumbo.

Vidonda vya tumbo vinatibika kirahisi ila vikicheleweshwa bila kutibiwa huweza kusababisha tatizo kubwa. Ni tatizo linalotesa sana na kuwanyima raha watu wengi, linahitaji umakini na pia husababisha magonjwa mengine kama kansa, amoeba (amiba), homa, kupungua uzito.

AINA ZA VIDONDA VYA TUMBO

Kuna aina zipatazo mbili za vidonda vya tumbo.

  1. Vidonda vya tumbo kubwa (Gastric ulcers) – Hivi ni vidonda vya tumbo vinavyotokea ndani kwenye tumbo kubwa.

 

  1. Vidonda vya utumbo mdogo (Duodenal ulcers) – Hivi ni vidonda ambavyo hutokea kwenye utumbo mdogo (hasa juu) duodenal-ulcer.

  

CHANZO CHA VIDONDA VYA TUMBO

Vidonda vya tumbo vina vyanzo tofauti ila vyote ni vile vinavyohusiana na mmeng’enyo wa chakula; vyanzo hivyo ni;

  1. Bakteria waitwao Helicobacter Pylori (H. Pylori)
  2. Matumizi ya dawa za kupunguza maumivu kama asprin
  3. Kuwa na mawazo mengi
  4. Kula vyakula vinavyozalisha acid kwa wingi
  5. Kunywa pombe na vinywaji vikali
  6. Uvutaji wa sigara
  7. Kutokula mlo kwa mpangilio

 

DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO

Dalili za vidonda vya tumbo hujitokeza baada ya kula au kabla ya kula, ila mara nyingi wengi huwa wanazipuuzia na kuendelea kukuza tatizo. Vidonda vya tumbo vina dalili kama;

  • Gastrita
  • Kupata maumivu ya tumbo yanayokuwa kama ya moto (kuunguza) baada na kabla ya kula
  • Kupatwa na kiungulia karibu na chembe ya moyo
  • Tumbo kujaa gesi na kuvimbiwa
  • Kichefuchefu na kutapika, tena yawezekana kutapika damu
  • Kupata haja kubwa ya rangi kahawia au nyeusi yenye harufu mbaya sana, pia haja yaweza kuchanganyikana na damu
  • Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito
  • Kushindwa kupumua vizuri

 JINSI YA KUEPUKANA NA VIDONDA VYA TUMBO

  • Kunywa maji mengi
  • Punguza mawazo. Fanya mazoezi yatakayokuepusha na mawazo
  • Punguza kiwango cha halemu (choresterol)
  • Usivute sigara
  • Punguza au acha kunywa pombe
  • Kula vizuri vyakula bora hasa asilia na sio vyakula vyenye kemikali
  • Lala vizuri kwa muda mzuri – masaa 7 hadi 9

TIBA YA VIDONDA VYA TUMBO

Tatizo la vidonda vya tumbo linatibika kufuatana na muda wa tatizo, mara nyingi wagonjwa wamekuwa wakidharau dalili za vidonda vya tumbo na kudhani kuwa hakuna madhara makubwa.

Tiba ya vidonda vya tumbo huwa ni antibiotiki ambayo hulenga kutibu maambukizi ya bakteria yaliyosababisha vidonda hivyo.

Kama vidonda vya tumbo vimesababishwa na dawa, daktari wako anaweza kukushauri kuhusu hatari na manufaa ya kutumia hizo dawa. Haishauriwi kutumia maziwa mabichi au almaarufu “maziwa fresh” kama tiba ya vidonda vya tumbo. Maziwa hupunguza maumivu ya tumbo kwa muda mfupi lakini husababisha asidi tumboni kuongezeka.

Baadhi ya dawa husaidia kupunguza kiwango cha asidi inayozalishwa tumboni. Hizi zinahitajika wakati kidonda bado kinapona. Kama vidonda vinatoa damu au vinasababisha shimo kwenye utumbo, upasuaji wa dharura unaweza kuhitajika. Hii athari hutokea kwa nadra.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags