Fahamu kuhusu biashara ya viatu ilivyo na faida

Fahamu kuhusu biashara ya viatu ilivyo na faida

Oooooooh! Niaje niaje wale wanangu wasiopenda kuajiriwa yaani kuna wale vijana msimamo wao kila siku ni kujiajiri tuu haijalishi iwe biashara au ujasiliamali wenyewe wanasema chamsingi ni mdomo uende kinywani.

Sasa leo tumekuja kukujuza kuhusiana na biashara ya viatu ilivyo na faida kubwa licha ya baadhi ya watu kuizarau lakini ni bonge la chanzo cha pesa wenyewe wanasema hulali nanjaa maana kila siku watu wanavaa na wengi wao hupendelea kupendeza

Mjasiriamali yoyote anayefikiria kuanzisha biashara ya viatu ana uhakika wa kupata wateja kwa sababu kwa namna moja au nyingine kila mtu lazima anunue viatu.

Jambo la msingi katika biashara hii japokuwa wateja ni wa uhakika ni unatakiwa kujua unalenga kuuza kwa nani na kisha kuweka bei rafiki kwa kundi hilo. Mfano kwa mwanafunzi wa chuo wateja wake lengwa ni wanafunzi wenzake so anatakiwa aweke bei rafiki ili aweze kuendesha biashara yake na kupata faida

.

Hivyo kama mfanyabiashara wa viatu ambaye ana malengo ya kufanikiwa, ni muhimu kufanya haya:

  • Kujua Wapinzani

Ikiwa unataka kuanzisha duka la viatu utafiti ni muhimu ili kuweza kujua mtindo upi utafaa kuvipanga viatu vyako na kuwavutia wateja na biashara yako imepanga kujikita katika viatu gani (vya bei ndogo au kubwa) kulingana na mtaji.

Lakini kuna umuhimu mkubwa wa kujifunza kwa wapinzani wako ili kuwahamasisha ipasavyo wateja. Tembelea maduka ya wapinzani ili kuona namna wanavyofanya biashara, kisha orodhesha udhaifu na nguvu zao na hakikisha unafanya vizuri zaidi.

  • Kujua Eneo lako la biashara

Mara nyingi watu huvutiwa na bidhaa au mahitaji hasa pale ambapo wanakuwa wanayaona kwa urahisi. Hivyo ili kupata wateja wa kutosha jitahidi kuchagua eneo la biashara ambalo ni rahisi kufika, na kuna biashara nyingine mbalimbali zinafanyika kama vile karibu na migahawa, karibu na vituo vya usafiri nk.

  • Jua kujitambulisha kwa wateja wako/utambulisho mzuri

Siku zote wateja watakukumbuka kama kuna huduma walipata kwako na hakuna sehemu nyingine wanaweza kuipata. Hivyo kama muuzaji wa viatu hakikisha unajitengenezea utambulisho wako binafsi ambao utawafanya wateja wote wasisahau na kuwaelekeza wateja wengine kufika katika eneo lako la biashara.

Kwa mfano mfanyabiashara Frank Knows amepta umaarufu mkubwa kwenye mtandao wa Instagram kwa kuuza viatu kwa Shilingi 35,000 tu bei ambayo ni bei nafuu sokoni. Kutokana na wengi kumudu bei zake, mjasiriamali huyu amefanikiwa kufungua maduka zaidi jijini Dar es salaam na mikoani.

Hivyo hata wewe unaweza kufungua account yako ya Instagram ya biashara ambayo utatumia kujitambulisha na kujulikana Zaidi kama wakina fred vunjabei.

Haya haya wanangu na wafuatiliaji wa @Mwananchiscoop nawewe unaweza kujaribu kufanya biashara hiyo na kupata mafanikio makubwa ondoa ile ya kauli unayojiambia kuwa nitaweza nitaweza, mimi nakwambia utaweza anza leo I hope utafanikiwa cha muhimu Zaidi mtangulize mungu katika kila hatua yako.

 






Comments 1


  • Awesome Image
    Mustapha Mpapai

    Upo wap mkuuu naitaji kuazishaa hii biashara

Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags