Esma: Mapenzi hayachagui, hayabagui

Esma: Mapenzi hayachagui, hayabagui

Baada ya kuonekana ndoa na mahusiano mengi ya watu maarufu nchini kutodumu, Esma Platnumz ambaye ni dada wa mwanamuziki DiamondPlatnumz , ameachia ujumbe kwenye #InstaStory yake akidai kuwa mapenzi hayachagui wala hayabagui kwa hiyo ukipata muda yafurahie kwani majuto yake ni baadaye. Esma ameandika,

“Mapenzi yaache yaitwe mapenzi hayachagui hayabagui, Diva tuu yupo kila siku kwenye kipindi cha mapenzi na yanamliza itakuwa sie, kuna muda unaamua kutulia mwanamme anazingua na kuna muda mwanamke… basi tafrani ila cha msingi ukipata muda wa ku-enjoy mapenzi yako wee enjoy tuu majuto baadae”

Nikukumbushe kuwa Esma amewahi kuwa kwenye mahusiano na #PettMan ambaye ndiye mzazi mwenzie lakini pia amewahi kufunga ndoa na #Msizwa na kisha ndoa yao kuvunjika, kwa sasa Esma yupo penzini na manager wa msanii Mavokali, anayefahamika kwa jina la JembeOne.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags