Erasto Nyoni awasaidia nauli timu ya majimaji

Erasto Nyoni awasaidia nauli timu ya majimaji

Beki wa kati wa klabu ya Simba SC Erasto Nyoni  baada ya Timu ya Majimaji ya Songea kukwama jijini Dar es Salaam kwa kukosa pesa ya nauli na deni la Hoteli alifanikiwa kuwasaidia kulipa na kuwapa Tsh. Milioni moja ambayo wamefanya nauli ya kurejea Songea.

Nyoni ambaye ni Mwenyeji wa Songea  alifunguka kupitia njia ya simu katika mahojiano na moja ya chombo cha habari na kueleza kuwa amewahi kupita hali kama hiyo, hivyo ameamua kuwapa support ili kuwatia moyo.

“Sisi kama Kaka zao tunatakiwa tuwaoneshe na tuwape moyo ili waweze kupambana maana kazi yetu ya mpira ni kazi ngumu sana unatakiwa usikate tamaa uwe Mvumilivu sasa uvumili hauji tu hivihivi lazima kuna Watu wawe wanakupa hiyo nguvu” amesema Nyoni

Aidha mwanasoka huyo alimalizia kwa kusema kuwa“Nimeshawahi kupitia hii hali ndio maana ilipotokea ikanisukuma  kufanya hivi kwasababu imeshawahi kunitokea” amsema Erasto






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags