Eminem ana jambo lake ijumaa hii

Eminem ana jambo lake ijumaa hii

Mwanamuziki kutoka Marekani Eminem ametangaza ujio wa wimbo wake mpya ambao utaachiwa siku ya Ijumaa Mei 31, 2024 alioupa jina la ‘Houdini’.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Eminem ame-share video akiwa anazungumza na mwanamazingaombwe (magician) kutoka nchini humo David Blaine kuhusiana na ujio wa ngoma yake mpya.

Aidha imeelezwa kuwa kumuweka Blaine katika kutangaza tarehe yake ya kutoa wimbo huenda ikawa ni ishara ya kuwajulisha mashabiki wake kuwa ngoma hiyo itakuwa kali na yakutisha.

Eminem anatarajia kuachia album yake mpya iitwayo ‘The Death of Slim Shady (Coup de Grâce)’ katika msimu huu wa joto huku wimbo wa ‘Houdini’ ikitajwa kuwa ndio ngoma iliyobeba album hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags