Ikiwa ni wiki mbili tu tangu Elon Musk ainunue kampuni ya Twitter, wafanyakazi wa kampuni hiyo wanaendelea kuuona moto wa mtu huyo tajiri zaidi duniani.
Katika barua pepe aliyotuma kwa wafanyakazi, tajiri huyo anayeendelea kutingisha kampuni yake anasema kila mfanyakazi anatarajiwa kufanya kazi akiwa ofisini kwa masaa yasiyopungua 40 kwa wiki, akifutilia mbali utaratibu wa kufanyia kazi nje ya ofisi.
Siku moja tu iliyopita bilionea huyo aliwafuta kazi wafanyakazi wote wa Twitter Afrika na kubakisha mfanyakazi mmoja Tu.
Chanzo BBC
Leave a Reply