Elon Musk airejesha akaunti ya Twitter ya Trump

Elon Musk airejesha akaunti ya Twitter ya Trump

Mmiliki mpya wa mtandao wa kijamii  wa Twitter Elon Musk ameirejesha akaunti ya Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump. Hayo yameelezwa  na mmiliki mpya wa kampuni hiyo.

Akaunti ya Trump iliyokuwa imefungwa kwa muda wa miezi 22, ilionekana tena kwenye mtandao huo juzi Jumamosi.

Elon Musk, mmiliki mpya wa mtandao wa kijamii wa Twitter aliendesha kura ya maoni, ambapo watumiaji milioni 15 wa Twitter walipiga kura, huku asilimia 51.8 wakipiga kura ya ndiyo ili kuwezesha kurudisha akaunt hiyo.

Ikumbukwe kuwa  akaunti ya Trump ilisimamishwa mwezi Januari, 2021, siku mbili baada ya wafuasi wake kuyavamia majengo ya bunge la Marekani na kusababisha kikao cha bunge la pamoja kusitishwa pamoja na vifo vya watu watano.

Wafuasi hao walikuwa na nia ya kuzuia kupitishwa matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2020 yaliyompa ushindi Rais wa sasa wa Marekani Joe Biden. Hivi majuzi, Trump alitangaza nia yake ya kugombea tena urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2024.

Mapema jana, Trump amesema hana haja ya kurejea kwenye Twitter na badala yake atasalia katika mtandao wake wa kijamii aliyouanzisha wa "Truth."

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags