Dubai yaondoa ushuru wa pombe

Dubai yaondoa ushuru wa pombe

Dubai imeondoa ushuru wake wa asilimia 30 kwenye pombe ikiwa ni jitihada za kukuza utalii ambapo pia itaacha kulipisha pesa ya ada kwenye leseni binafsi ya pombe ambayo alitakiwa kuwa nayo yeyote anayetaka kununua pombe, mabadiliko haya yatadumu kwa kipindi cha mwaka mmoja wa majaribio.

“Kwa kuondolewa kwa asilimia 30 ya ushuru wa Manispaa na leseni ya bure ya pombe, kununua vinywaji unavyopenda sasa ni rahisi na kwa bei nafuu kuliko hapo awali" Mmoja wa Wasafirishaji wakuu wa pombe Dubai” ameandika katika mtandao wake.

Baadhi ya mitandao ya Dubai imeripoti kuwa imefanya hivi ili kukabiliana na ushindani unaoletwa na Majirani zake ambao wameweka masharti nafuu kwenye sekta za starehe na hoteli na kuwavutia Wakazi wa Dubai kuendesha magari hadi kwenye hizo falme nyingine na kununua pombe kwa wingi.

Inaelezwa kuwa Watu wasio Waislamu nchini Dubai hutakiwa kuwa na angalau umri wa miaka 21 ili kuruhusiwa kunywa pombe na hutakiwa pia kubeba leseni ya pombe iliyotolewa na Polisi.

Oooooooh! kwahiyo sahizi kwa wenzetu ni mitungii mitungii, kibongo bongo ungependa serikali iondoe ushuru wa nini? dondosha komenti yako hapo chini mwanangu sana.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags