Drake & Taylor wachuana tuzo za Billboard

Drake & Taylor wachuana tuzo za Billboard

‘Rapa’ kutoka nchini Marekani Drake na mwanamuziki mwezie Taylor Swift wanashikiria rekodi ya ushindi wa muda wote katika Tuzo za muziki za Billboard (BBMAs) baada ya kila mmoja kushinda tuzo 39.

Hii inakuja baada ya siku ya jana msanii Tylor Swift kushinda tuzo 10 mfululizo na kufikia jumla ya tuzo 39 katika career yake ya muziki, huku Drake akishinda tuzo 5 na kufikisha jumla ya tuzo 39.

Tylor Swift aliweza kuibuka na tuzo mbalimbali ambapo moja wapo ikiwa ni ya msanii bora wa kike. Tuzo za Billboard Music Awards Sunday night, zilifanyika siku ya Jumapili kwa njia ya mitandao ambapo wasanii wengine walioshinda tuzo katika usiku huo ni SZA, Miley Cyrus, Jung Kook, Bebe Rexha, Tate McRae na Mariah Carey.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags