Drake ndiye mmiliki wa pete ya Tupac

Drake ndiye mmiliki wa pete ya Tupac


Nyota wa muziki kutoka Marekani Drake amewaacha watu kwenye maswali yasiyokuwa na majibu, baada ya ku-post kwenye #InstaStory yake picha ya pete inayofanana na iliyokuwa ikimilikiwa na nguli wa muziki wa Hip-hop marehemu Tupac.

Pete hiyo yenye mchaganyiko wa madini ikiwemo dhahabu, rubi na almasi ambayo ilikuwa iliuzwa kwenye mnada maalumu hip-hop huku ikidaiwa kuwa iliuzwa kwa rekodi ya dola million 1 ambayo ni zaidi ya TZS Bilioni 2 sasa imeonekana mikononi mwa Drake ingawa mnunuzi wa pete hiyo hakuwekwa wazi.

Inaelezwa kuwa mbunifu wa pete hiyo alikuwa Tupac mwenyewe, ambapo kwenye muonekano wake ina muundo wa taji/ kofia ya kifalme na maneno yasomekayo "Pac & Dada 1996," kama heshima ya penzi la Pac na aliyekuwa mpenzi wake Kidada Jones.

Mara ya mwisho pete hiyo kuonekana kwenye kidole cha #Pac ilikuwa mwaka 1996 kwenye Tuzo za Muziki za Video za MTV, ikiwa ni siku tisa tu kabla ya kupigwa kwake risasi akiwa Las Vegas.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags