Baada ya kutolewa kwa taarifa kuwa kutakuwa na burudani wakati wa mapumziko kwenye Kombe la Dunia, na sasa Rais wa FIFA, Gianni Infantino ameonesha nia ya kumtaka Drake kutumbuiza katika mchezo huo.
Wakati alipokuwa kwenye mahojiano ya ‘Good Day New York’ na mtangazaji Rosanna Scotto ambaye alimshauri Infantino kumchukua rapa huyo kutoka Canada ili kurudisha mashambulizi kwa Kendrick Lamar, ambaye alitumbuiza kwenye Super Bowl LIX.
“Nina wazo zuri kwa ajili yako kwa ajili ya halftime, unaweza kumchagua Drake kwa sababu Kendrick Lamar alimkashifu kwenye Super Bowl, na Infantino, akajibu.
Hivyo tunaweza kuunda aina fulani ya ushindani?, hilo ni wazo zuri kwa kweli Drake alikuwa pamoja nasi tulipotangaza wenyeji wa mashindano hayo, nadhani nimehifadhi namba ya Drake mahali Fulani nitamtafuta,” amesema Infantino
Kupitia mitandao ya kijamii mashabiki walijibu na kuzua mijadara kuwa onyesho la Drake kwenye Kombe la Dunia litakuwa bora na kubwa kuliko onyesho la Kendrick Lamar kwenye Super Bowl, huku wengine, hasa Wamarekani, wakipuuza wazo hilo.
Ingawa onyesho la Drake halijathibitishwa, Chris Martin na Phil Harvey wa Coldplay wameteuliwa kuwa wasimamizi wa Halftime Show ya kwanza kabisa ya Kombe la Dunia, ambayo inatarajiwa kufanyika 19 Julai 2026 kwenye MetLife Stadium huko New Jersey.
Ikumbukwe Rais wa FIFA, Gianni Infantino, Machi 5, 2025 kupitia ukurasa wa Instagram wa, alitoa taarifa ya kuwepo kwa burudani ya muziki katika kipindi cha mapumziko kwenye fainali za kombe la dunia 2026.
“Ninaweza kuthibitisha onyesho la kwanza kabisa la muda wa mapumziko kwenye fainali za kombe la dunia la FIFA, kwa ushirikiano na Global Citizen. Huu utakuwa wakati wa kihistoria kwa Kombe la Dunia na FIFA na onyesho linalolingana na tukio kubwa zaidi la michezo ulimwenguni,” aliandika Infantino.
Hatua hii ya FIFA kutumia muda wa mapumziko kutoa burudani ya muziki kwenye fainali za kombe la dunia 2026 limekuja kufuatia Super Bowl Half Time Show ya mwaka 2025 aliyotumbuiza Kendrick Lamar kuacha alama kubwa kwenye ulimwengu wa burudani huku ikiongeza thamani ya mchezo husika.

Leave a Reply