Drake apewa ufunguo wa heshima

Drake apewa ufunguo wa heshima

Mwanamuziki kutoka nchini Canada Drake amepewa ufunguo wa heshima huko Memphis katika Kaunti ya Shelby mahali apozaliwa Baba.

Mkali huyo mara kadhaa amekuwa akitaja 901 katika mashairi yake kama sehemu ya kuenzi mahali ambapo aliishi wakati wa majira ya joto akiwa mtoto.

Mwenyekiti wa Kaunti ya Shelby, Mickell Lowery alitoa heshima hiyo Juni 26 huku akimwambia, “Tunapenda watu wetu, Muziki wa Memphis unagusa dunia. Una damu ya watu wengi wa Memphis ndani yako na hakika unagusa dunia’’

 
Mickell aliendelea kumshukuru Drake kwa kuiweka Memphis katika ramani ya Dunia kupitia muziki wake na kuongeza, “Hii inapaswa kuwa karibu na moyo wako kwa sababu ni kutoka 901”

Vile vile mwenyekiti huyo aliongeza kuwa kaunti hiyo inautaratibu wa kutambua mchango wa watu mbalimbali mahali hapo kwa kutoa heshima kama hiyo, “Watu wetu tunawathamini sana.” Kisha Drake kwa utani alimuuliza baba yake, “Baba, umeshapata hii?”, na mzee Dennis Graham alijibu, “Walinipa ufunguo kwenye hoteli wa barabara hii.”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags