DR CHENI: Hongera Nandy na Billinass kwa kupata mtoto

DR CHENI: Hongera Nandy na Billinass kwa kupata mtoto

Aloooooooh! Yaani week hii ni ya taarifa nzuri tuu, inasemekana mambo yamejibu huko bwana, kutoka kwa yule MC aliyesherehesha katika siku ya harusi ya taifa ya Nandy na Billinass, MC Dr Cheni ameweka wazi na kusema kuwa wawili hao wameshapata mtoto tayari.

Dr. Cheni ameyaeleza hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akiambatanisha picha ya siku ya harusi ya Nandy na Billinas kwa kuandika kuwa “woow congratulations Mr and Mrs Billnass na Nandy kwa kupata mtoto, Mungu awalindie kitoto chenu, mbarikiwe sana,” ameandika Dr Cheni.

Hata hivyo, wawili hao (Nandy na Billnass) hawaconfirm kama habari hizo ni za ukweli au la.

Basi bwana mwanangu wa Mwananchi Scoop tutaendelea kuwajuza taarifa zaidi kuhusiana na mtoto kama ni wa kike au wa kiume, na kama kweli tayari mambo yamejipa. Endelea kufuatilia mitandao yetu ya kijamii kwa taarifa zaidi.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags