Muigizaji Maarufu kutoka Marekani 'Djimon Hounsou' amweka wazi hali ya chumi na kutothaminiwa kwenye tasnia ya filamu Hollywood baada ya kufanya mahojiano na CNN nakufichua kuwa, licha ya kazi yake iliyochukua zaidi ya miaka 20 na kusifiwa kwa umahiri wake wa kuigiza, anaendelea kukabiliwa na changamoto za kifedha huko Hollywood.
Djimon ambae amezungumza hayo kwenye kipindi cha "African Voices Changemakers" cha CNN, nakuelezea masikitiko yake kuhusu malipo kidogo anayopokea na kutothaminiwa katika tasnia ambayo ameifanya kwa muda mrefu.
"Bado ninapitia changamoto kupata riziki, Nimekuwa katika biashara hii ya kutengeneza filamu sasa kwa zaidi ya miongo miwili na nimeteuliwa kuwania tuzo za Oscar mara mbili , nimekuwa katika filamu nyingi kubwa, lakini bado ninatatizika kifedha. Ninalipwa kidogo.” Hounsou alikiri.
Hounsou, ambae amejipatia umaarufu zaidi kupitia kazi za filamu kama vile Gladiator, Amistad, Blood Diamond, alikosoa tasnia ya filamu kwa kile anachokiona kama ubaguzi wa kimfumo na chuki kwa waigizaji wakigeni.
Leave a Reply