Dili ya boga la vanilla hili hapa

Dili ya boga la vanilla hili hapa

Kumekucha tenaaa!! Mambo vipi mtu wangu kama kawaida kwenye ukurasa wa Nipe Dili bhana mimi naendeleza mautundu yangu ya kukupa kile unachostahili.

Ikiwa tuko mbioni kuukamilisha Mwezi mtukufu wa Ramadhani, hivi umeshapika futari ya boga la vanilla lenye nazi weyee? Aah acha kabisa najua mate yanakudondoka hapo.

Boga ni moja kati ya futari pendwa sana katika familia nyingi za wale wanaopenda kula vitu vya asili hupendelewa mnoo kwani huliwa sana katika kipindi hiki cha mfungo.

Sasa wiki hii kwenye Nipe Dili tunaingia jikoni rasmi kufundishana  jinsi ya kupika boga la nazi haswaaa! Mwanamke mapishi hasa ukiyajua au vipi? Karibu.

Tuingie jikoni sasa jinsi ya kupika Boga mahitaji muhimu

  • Boga lenyewe 1.
  • Nazi 1.
  • Sukari kijiko kikubwa cha chakula vitatu au zaidi kulingana na uhitaji wako wa sukari kwenye boga lako.
  • Hiliki kijiko cha chai, raha ya boga linukiee haswaa!.
  • Vanilla ya maji vijiko vikubwa viwili.

Namna ya kutayarisha na kupika

  • Menya boga kiasi ukitakacho
  • Kisha kata vipande vya saizi tu yaani visiwe vidogo sana wala vikubwa sana, maana ukikata vidogo sana vitarojeka.
  • Kisha andaa sufuria yako nzuuri ambayo itatosha kuchemshia boga lako, chemsha mpaka yaive vizuri weka maji ya saizi ambaye yatawezesha kuiva.
  • Maji yakishakauka sasa ni wakati wako wakuweka hiliki na sukari kulingana na boga uliloliandaa.
  • Kisha unamimina tui la nazi ambapo utaweka tui lile la pili kwanza halfu utamalizia tui bubu lenyewe.
  • Utaacha ichemkie kabla ya kukauka tui utaepua na hapo futari yetu ya boga itakua tayari.
  • Masha’allah hivyo ndivyo ninavyomalizia najua hapo harufu utakayoipata si ya kawaida na utamu uliojee!! Jikaze usije kufungua swaumu bureee ahsantee zingatia hayo mambo yatakua vizuri kabisaaa!!

Tuambie lako utatengeneza lini? Nasubiri comment zako!






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags