Dili la kutengeneza ice-cream za ubuyu

Dili la kutengeneza ice-cream za ubuyu

Aaaah !!!! wewe uhali gani msomaji wa kipengele konki kabisa cha Nipe dili? Bila shaka uko biyeee kabisa na unapambana na michakato ya kimaisha ndo inavyotakiwa kabisa. 

Kama hujui nini chakufanya basi always nipe dili inajukumu la kuhakikisha hukosi mlango wa kutokea kila kukicha bhnaa hakuna kuishi kizembe.

Yap leo nakuletea hadi machoni mwako dili hili hapa lakuingiza mia mia kwa siku ushindewe wewe tu kuchangamkia fursa hii hapa twende sawa nakupa maelekezo jinsi ya kuwin kwenye utengenezaji wa lambalamba za ubuyu na Ice cream ndani yake.

Twende kazi mahitaji sasa haya hapa.

Ubuyu wa unga ½

Sukari ¾

Ngano vijiko viwili 2

Rangi yoyote inayokuvutia ruksaa 

Maji lita 8-10

Usisahau Vanilla au Hiliki. 

Kwa mahitaji hapo tumekamilika nilikwambia ni simple sana, sasa twenzetu kwenye utengenezaji wenyeweeee!!

Tunaanza sasa weka maji, weka ubuyu wa unga nusu kilo, hakikisha ubuyu wako umeuchanganya kabisa na unga wa ngano vijiko 4.

Kisha bandika jikoni huku ukikoroga mpaka uwe mzito kiasi halafu chota hata sehemu ili kuweka rangi tofauti, koroga kwa dakika 5.

Baada ya hapo shughuli imeisha epua kisha uache upoe, ruksa fanya mchakato wa kupaki kwenye vifungashio vyako.

Angalizo:  Unga wa ngano unafanya ice cream kuwa laini isiwe ngumu badala ya ngano unaweza weka corn flour.

Ayeyeeeee tumemaliza kazi ni kwako mpambanaji wangu!!!!!!!!.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags