Dili la kupika Bagia za dengu hili hapa!

Dili la kupika Bagia za dengu hili hapa!

Weuwee! Salamu hizi unazipata kwenye magazine ya Mwanchi Scoop pekeee au sio say aye yeee kama kawaida tuko kimadili zaidi kuliko mengine mwanangu mwenyewe.

Na leo bwana tutaelekeza namna ya kuandaa bagia za dengu kama ifutavyo wewe tu na ufuatiliaji wako wa series hii ya Nide dili karibu. 

Mahitaji

Unga wa dengu nusu

Chumvi kijiko cha chai

Maji baridi- 1 glass.

Baking Powder- 1 cha chai

Majani ya kotmiri yaliyokatwakatwa- kiasi

Kitunguu maji kilosagwa- 2 kijiko cha supu.

Kitunguu saumu( thoum) ilosagwa au ya Unga- kijiko cha chai mafuta kadiria.

Namna ya kutayarisha na Kupika sasa

Sasa tumia bakuli lenye nafasi mimina unga na viungo vyote, tumia uma au kijiko kuvuruga mchanganyiko, kisha ukiwa laini bila mabuja hakikisha sio mzito na sio mwepesi uwe kiasi 

Uwache mchanganyiko wako kwa muda war obo saa dakika 15 hadi 20.

Weka karai jikoni au sufuria nzito ndogo, tia mafuta na acha yapate moto sawasawa.

Tumia kijiko cha chakula kuchota unga kutia kwenye mafuta unapotia hakikisha kipimo chako chote kimelenga sehemu moja bila ya kutandaza ili uweze kupata umbo maalumu.

Unazigeuza upande wa pili umalize zikiiva na kuwa rangi ya brown mpauko.

Tumia chombo chenye matundu ili kuchuja mafuta baada ya kuchoma kisha badilisha kwenye sahani au bakuli nyingine tayari kuliwa inaweza kuliwa na tomato sauce, chachandu au kachumbariiiii.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags