Diddy azidi kuyakanyaga, afunguliwa kesi nyingine

Diddy azidi kuyakanyaga, afunguliwa kesi nyingine

Mkali wa Hip-hop kutoka Marekani Diddy anakabiliwa na kesi nyingine ya unyanyasaji wa kingono ambayo imefunguliwa hivi karibuni na mwanamitindo wa zamani Crystal McKinney, tukio linalodaiwa kutokea 2003 huko New York City.

Kwa mujibu wa tmz imeeleza kuwa McKinney alipokuwa na miaka 22 alialikwa kwenye hafla ya wiki ya mitindo ya wanaume huko Cipriani Downtown ambapo alikutana na Combs, wakati wa sherehe mwanadada huyo alikwenda bafuni na kudai kuwa Diddy alimfuata na kumlazimisha kufanya ngono kwa kutumia mdomo.

Aidha katika maelezo ya mwanamitindo huyo aliendelea kwa kudai kuwa rapa huyo alitumia nguvu mpaka kupelea kuzimia, ambapo baada ya kurejesha fahamu alingundua kuwa alishambuliwa kingono.

Hata hivyo, kesi hiyo haijaweka wazi kama ni yamadai ya kulazimishwa kufanya ngono ya mdomo au kushambuliwa kingono alipokuwa amepoteza fahamu.

Crystal McKinney amedai kuwa kufuatia na tukio hilo alipata msongo wa mawazo na kutaka kujiua kwa zaidi ya mwaka hivyo amefungua kesi hiyo kutaka kulipwa fidia ya udhalilishaji huo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags