Diddy Arudisha Mashambulizi, Afungua Kesi

Diddy Arudisha Mashambulizi, Afungua Kesi

Baada ya kuandamwa na kesi mfululizo za unyanyasaji wa kingono, hatimaye rapa Diddy ameamua kurudisha mashambulizi. Anadaiwa kufungua kesi ya madai kwa mtu aliyedai kuwa na video chafu za msanii huyo.

Kesi hiyo, iliyowasilishwa na mawakili wa Combs jana Januari 22, 2025 jijini New York imeeleza kuwa washtakiwa ambao ni wamiliki wa News Nation walitunga na kuzua madai ya uongo kuhusiana na kumiliki video za Diddy akiwadhalilisha mastaa wenzake.

“Sean ‘Diddy’ Combs amechukua msimamo dhidi ya uongo wa kimakusudi uliozushwa na kuenezwa na watu wanaotafuta kunufaika kwa gharama yake. Washtakiwa hawa wametunga na kusambaza uongo wa kushangaza kwa kupuuza ukweli kwa makusudi.

Uongo wao umeharibu mtazamo wa umma na kuathiri jamii kwa kiasi kikubwa. Malalamiko haya yanapaswa kuwa onyo kwamba uongo wa kimakusudi kama huu, unaoathiri haki ya Bw. Combs kupata kesi ya haki, hautavumiliwa tena,” amesema Erica Wolff, wakili wa Combs.

Aidha rapa huyo amewasilisha kesi hiyo chini ya mawakili wake akidai fidia ya dola milioni 50 ikiwa ni zaidi ya Sh 125 bilioni dhidi ya Ariel Mitchell, Nexstar Media na Courtney Burgess.

Ikumbukwe kuwa Combs alikamatwa kwa mara ya kwanza Septemba 16,2024 jijini New York katika moja ya hoteli iliyopo jijini humo, akikabiliwa na tuhuma za unyanyasaji wa ngono, usafirishaji haramu wa watu huku kesi yake ikianza kusikilizwa Mei 5, 2025. Kwa sasa rapa huyo amezuiliwa katika gereza la MDC Brooklyn






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags