Diddy anamchango wake kwenye mtandao wa X

Diddy anamchango wake kwenye mtandao wa X

Mkali wa Hip-hop Marekani Diddy ametajwa kuwa ni mmoja wa wawekezaji waliomsaidia Elon Musk kununua mtandao wa X (zamani twitter) mwaka 2022.

Kwa mujibu wa tovuti ya Tmz imeeleza kuwa kufuatia na orodha iliyotolewa mapema wiki hii ikiorodhesha mashirika 100 yaliyosaidia kufanikisha Elon kununua ‘X’, Diddy ni mmoja wapo akiwa chini ya kampuni yake ya ‘Sean Combs Capital, LLC'.

Licha ya kutajwa kutoa mkwanja mrefu katika uwekezaji huo lakini mpaka kufikia sasa bado haijawekwa wazi ni kiasi gani hasa Diddy amechangia katika kununua mtandao huo huku mpaka Agosti 2024 bado haijajulikana nani anamiliki hisa zaidi kwenye kampuni hiyo.

Wawekezaji wengine walioorodheshwa ni pamoja na Bill Ackman, Kiongozi wa Saudia Al Waleed bin Talal Al Saud na mwanzilishi wa Twitter, Jack Dorsey.

Elon Musk na Diddy wanadaiwa kuwa marafiki wa muda mrefu na walionekana pamoja kwa mara ya kwanza katika onesho la vichekesho la ‘Dave Chappelle' mwaka 2022, lakini kwa sasa wanatajwa kupeana visogo baada ya Combs kuandamwa na kesi za unyanyasaji wa kingono.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags