Diddy akabiliwa na kesi  mpya 120, unyanyasaji wa kingono

Diddy akabiliwa na kesi mpya 120, unyanyasaji wa kingono

Mkali wa Hip-Hop wa Marekani Sean “Diddy” Combs ameripotiwa kuhusishwa katika kesi mpya 120 za unyanyasaji wa kingono zinazotarajiwa kuwasilishwa mahakamani siku 30 zijazo kabla ya kesi zake za awali kuanza kusikilizwa.

Wakati akiongea na waandishi wa habari jana Oktoba 1, wakili Tony Buzbee kutoka Texas ameweka wazi kuwa watu 120 wamewasilisha madai ya unyanyasaji wa kingono yaliyodaiwa kufanyika miaka 20 (miongo miwili) iliyopita huku akisema kuwa ana ushahidi wa picha na video.

“Tutawafichua wale waliowezesha mwenendo huu kwa siri. Tutafuatilia jambo hili bila kujali ushahidi utamhusisha nani, watu wengi wenye nguvu, siri nyingi chafu, timu yangu imekusanya picha, video, na ujumbe wa maandishi.

“Orodha ni ndefu tayari, lakini kwa sababu ya asili ya kesi hii, tutahakikisha kabisa kuwa tuko sahihi kabla ya kufanya hivyo majina haya yatakushangaza.” Buzbee alisema wakati akiwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari.

Aidha wakili huyo alimtaja mhusika mmoja kuwa ni mtoto mwenye umri wa miaka tisa ambapo Diddy na wengine walimnyanyasa kingono katika studio za Bad Boy Records huko New York City.

Buzbee anadai Diddy alimshawishi mvulana huyo wa miaka 9 kwenda kwenye usaili kwa ahadi ya kumpa mkataba wa muziki, na kisha akamnyanyasa kingono.

Hata hivyo kwa mujibu wa wakili huyo baadhi ya watu mashughuli watajumuishwa kwenye kesi hizo huku akidai kuwa atawashitaki kwa kuhusika au kuujua ukweli na kuukalia kimya.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags