Diamond ampeleka tena mjini Mama yake kwenye video

Diamond ampeleka tena mjini Mama yake kwenye video

 Imekuwa kawaida kuona wanamuziki wakitumia wapenzi wao kama video vixen au video king kwenye video zao, na kama maudhui ya wimbo ni kuhusu mama basi wengi hutumia mama wa kukodi.

Lakini hii imekuwa tofauti kwa nyota wa muziki wa #BongoFleva #DiamondPlatnumz kwa mara ya pili sasa anamtumia mama yake kwenye video za nyimbo.

Awamu hii #Simba amemtumia mama yake kwenye video ya wimbo mpya wa Jux uitwao #Enjoy ambao #Diamond ameshirikishwa humo ndani.

Huenda video hiyo ikapata watazamaji wengi kutokana na mama Dangote kuwepo humo ndani, kama ilivyokuwa kwenye wimbo wa utanipenda  ambao pia #Diamond alimtumia mama yake katika video ya wimbo huo, ambao hadi sasa una watazamaji 26M kwenye mtandao wa #Youtube.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags