Diamond akimbiza kwenye mirabaha, Zuchu aongoza wanawake

Diamond akimbiza kwenye mirabaha, Zuchu aongoza wanawake

Yale maokoto ambayo wengi walikuwa wakiyasubiri kwa muda mrefu ili kujua kiasi cha pesa ambacho wasanii watapata kutokana na kazi zao kupigwa kwenye vituo mbalimbali vya Redio na Tv usiku wa kuamkia leo yalitoka.

Serikali kupitia Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) usiku wa kuamkia leo waliongoza zoezi hilo la utoaji Mirabaha kwa wasanii. Katika maokoto hayo #Diamond anaonekana kushikilia usukani wa kuwaongoza wasanii wengine, #Diamond ameondoka na Sh milioni 7.7.

Huku katika maokoto hayo msanii aliyefatia kwa kuondoka na mkwanja mrefu ni King Kiba kaondoka na Sh milioni 5, Rayanny Sh milioni 4.5, Mboso Sh milioni 4.2 na Harmonize Sh milioni 3.4 , upande wa wasanii wa kike Zuchu ameshika usukani kwa kuondoka na milioni 4.7,akifuatia Nandy milioni 3.5, na Maua Sama milioni 2.3, kwenye #HipHop #Mbuzi Young Lunya hajakaa kinyonge kaondoaka na milioni 1.6.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags