Diamond aandaa zawadi kwa mashabiki

Diamond aandaa zawadi kwa mashabiki

Baada ya kuachia ngoma ambayo inafanya vizuri kwenye mitandao ya kijamii hususani #YouTube, mwanamuziki Diamond ameonesha mzigo wa mavazi wenye jina la wimbo wake wa ‘Mapozi’ ambao amemshirikisha Mr Blue na Jay Melody.

Diamond amerudi na mavazi hayo akitokea Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya promo ya wimbo wake, ambapo nguo hizo amepanga kuwapa mashabiki wake wa Instagram, Snapchart, TikTok ambao wamekuwa 'wakimsapoti' kila siku.

Aidha licha ya hayo Simba ameeleza kuwa anatarajia kutoa ngoma nyingine kabla ya Ramadhani. Wimbo wa ‘Mapozi’ hadi kufikia sasa kwenye mtandao wa YouTube unazaidi ya wasikilizaji milioni mbili ukiwa na siku saba tangu kuachiwa kwake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags