DC aonya wanawake kutembelea wanaume wasio wajua.

DC aonya wanawake kutembelea wanaume wasio wajua.

Mkuu wa wilaya ya Njombe, Kissa Kasongwa ametoa rai kwa wanawake kupunguza ujasiri wa kwenda kwa wanaume bila kujua vizuri ni mtu waina gani.

Ni baada ya Juma Msemwa  mwenye umri wa miaka 27, kukamatwa kwa tuhuma za kuwafungia ndani kwake wanawake 3 kisha kuwabaka na kuwalawiti kwa zamu, huku akiwa amewafunga kamba na kuwajaza vitambaa mdomoni kwa takribani wiki moja.

Shuhuda aliyefika wakati wa kukamatwa kwa kijana huyo amesema, alipata taarifa kwa mwanamke mmoja aliyetoroka kwenye nyumba ya Juma, akaenda kuomba msaada dukani akiwa na hali mbaya kwa kuwa Juma alikuwa anawabaka siku nzima na alipochoka aliwawekea gunzi au tango Sehemu za siri.

Aidha Kissa aliwashukuru wananchi kwa ushirikiano walioufanya mpaka kijana huyo kukamatwa

"Niwashukuru wananchi kwa kuwaokoa hawa wanawake bila ya huyu mmoja kujinasua huenda leo tungeongea mengine”alisema mkuu wa wilaya hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags