Davido anajambo lake mwaka huu

Davido anajambo lake mwaka huu

Mkali wa #Afrobeat kutoka nchini Nigeria, #Davido ameweka wazi kuwa album yake mpya tayari imekamilika na muda wowote inaweza kutoka.

#Davido ameweka wazi suala hilo wakati alipokuwa kwenye mahojiano na #Kaicenat ambapo alifunguka kwa kudai kuwa ameshamaliza kurekodi album yake mpya ambayo itakuwa na nyimbo 15 huku akieleza kuwa amefanya ‘kolabo’ na wasanii wa nje sita.

Lakini mpaka kufikia sasa haijawekwa wazi jina wala siku ya kutoka kwa alibumu hiyo, ikumbukwe kuwa Davido aliuanza mwaka kwa kushirikishwa katika remix ya ngoma ya Kizz Daniel iitwayo 'Twe Twe' na 'Easy On Me' ya Logos Olori.

Album ya mwisho kuachiwa na O.B.O ilikuwa Machi, 2023, iitwayo ‘Timeless’ albumu ambayo ilimrudisha tena kwenye mstari mwanamuziki huyo baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu kufuatiwa na kifo cha mwanaye #Ifeanyi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags