Davido ajigamba albamu ya Wizkid kubuma

Davido ajigamba albamu ya Wizkid kubuma

Na Masoud Kofii

Mwimbaji wa Afrobeats Davido, ameonesha kujigamba baada ya kuendelea kushikilia rekodi ya kuwa msanii pekee aliyeshika nafasi 16 kwenye chati ya nyimbo za juu za kila siku kwenye mtandao wa Spotify Nigeria, kwa siku mbili mfululizo licha ya albamu ya Wizkid kutoka hivi karibuni.

Albamu mpya ya Wizkid, 'Morayo' ilivunja rekodi kadhaa kwenye mtandao wa Spotify lakini nyimbo zake zimeshindwa kushika nafasi 16 za kwanza kwenye Chati ya Nyimbo za Juu za kila siku za mtandao huo. Hivyo imeshindwa kuvunja rekodi iliyowekwa na Davido kupitia albumu yake ya 'Timeless' mwaka uliopita

Kufuatia Wizkid kushindwa kuvunja rekodi ya Davido, jukwaa la ufuatiliaji wa muziki, The Data Dash liliandika kupitia X, “Davido anabaki kuwa msanii pekee aliyeshika nafasi 16 kwenye chati ya Nyimbo za Juu za kila siku ya Spotify Nigeria kwa siku 2 mfululizo, na nyimbo zote zikiwa mpya kutoka kwenye albamu yake ya 'Timeless'."

Kutokana na taarifa hiyo ya 'The Data Dash' imemfanya Davido ajigambe kwenye mitandao ya kijamii Davido na kuchapisha ujumbe, "Remain the only" akimaanisha"Bado ni yeye pekee"






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags