Dani Alves atupwa jela miaka minne na nusu kwa ubakaji

Dani Alves atupwa jela miaka minne na nusu kwa ubakaji

Nyota wa zamani wa Brazil, Dani Alves amehukumiwa kwenda jela miaka minne na nusu kwa kosa la ubakaji, hukumu hiyo iliyosomwa Leo Februari 22 katika Mahakama iliyopo nchini Hispania.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la AFP limesema Alves ametupwa jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka msichana mdogo wakati akiwa katika Club ya ‘Sutton’ iliyoko Barcelona, mwaka 2022.

Ikumbukwe kuwa Dani Alves alikuwa rumande tangu mwishoni mwa mwaka 2023 akisubiri hukumu hii, hata hivyo baada ya hukumu hiyo kusomwa anatakiwa kumlipa fidia mwanamke huyo ya euro 150,000 ambayo ni sawa na tsh 414 milioni.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags