Country wizzy;Kipaji changu kikubwa kuliko pesa nilizompa Harmonize

Country wizzy;Kipaji changu kikubwa kuliko pesa nilizompa Harmonize

Na Habiba Mohammed

Ebwanaaaaa! Mko good kama kawa kama dawa kwenye chochoro za entertaitment nimekusogezea mkalii wa mziki wa. Rap   Ibrahim Mandigo maarufu kama Country wizzy amefunguka na kusema kuwa anakipaji kikubwa kuliko pesa alizolipa kwa konde.

 Msanii huyu ambae amepitia menejimenti tofauti tofauti na wengi wetu tumemfahamu kupitia kwa Konde gang chini ya usimamizi wa Harmonize ,katika menejimenti hiyo msanii huyu aliweza kuachia nyimbo kadhaa ambapo alikaa chini ya uongozi huo kwa miaka miwili.

Msanii huyo katika mahojiano na moja ya chombo cha Habari amefunguka machache kuhusiana na yeye kutoka menejimenti ya konde gang na kupata stahiki zake kwa nyimbo alizofanya wakati yuko kwenye lebo hiyo.

 “Nashukuru nimeweza pata stahiki zangu zote za nyimbo ambazo nilifanya, sasa huu ndo wakati wangu wa kujitanua zaidi kimziki na kuleta radha na unyamwezi mwingi kwenye mzikii wa rap” amesema Country wizzy

Bwana katika mahojiano hayo mwanamziki huyu aliulizwa swali kuhusiana na malipo alioyalipa kwenye lebo ya Konde gang na kusema kuwa “Pesa ni nyingi siweze kusema how much naamini hizo pesa si chchote na kipaji nilicho nacho ,nina kipaji kikubwa kuzidi pesa nilizolipa konde gang” amesema rapa huyo

Aiseeeeee!haya haya wenzangu na mie ambao tuko na vipaji vyetu pesa ina nafasi gani katika kukuza kipaji chako? ama ndo uko tayari kuuza haki zako katika kipaji ulicho nacho ili upate pesa.?Shusha comment yako hapo chini.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags