Chris Brown akicheza ‘Komasava’ ya Diamond

Chris Brown akicheza ‘Komasava’ ya Diamond

Mwanamuziki kutoka Marekani Chris Brown bado ameendelea kuonesha mapenzi yake kwenye ngoma za wasanii wa Afrika na sasa ameonekana akicheza ‘Komasava’ ya Diamond aliyomshirikisha Chley na Khalil Harrison.

Hii si mara ya kwanza kwa msanii huyo kuvutiwa na wasanii wa Afrika wiki iliyopita kwenye ziara yake ya ‘11:11’ alitumbuiza na kucheza ngoma ya ‘Tshwala Bam’ iliyoimbwa na mwanamuziki kutoka Africa Kusini Titom aliyomshirikisha Yuppe.

Wimbo wa ‘Komasava’ (Comment Ça Va) unaendelea kuwa mkubwa duniani kote kutokana na wimbo huo kutaja Lugha za nchi mbalimbali ambapo siku chache zilizopita naye mwanamuziki kutoka Marekani Swae Lee alionekana akicheza wimbo huo huku Mataifa mbalimbali yakiendelea kuvutiwa na ngoma hiyo.

Kupitia mtandao wa Youtube ngoma hiyo inazidi kukimbiza ambapo mpaka kufikia sasa inazaidi ya watazamani milioni 2.7 ikiwa ni mwezi mmoja tuu tangu kuachiwa kwake.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags