China yatangaza kulegeza vizuizi vya Covid nchini

China yatangaza kulegeza vizuizi vya Covid nchini

Kutoka nchini China leo imetangaza kulegeza vizuizi vya kitaifa vya Covid kufuatia maandamano ya kupinga mkakati huo mkali ambayo yaligeuka kuwa miito ya kutaka uhuru zaidi wa kisiasa.

Chini ya muongozo mpya uliotangazwa na Tume ya Taifa ya Afya, kasi na upeo wa vipimo vya PCR, vitapunguzwa. Kufungwa kwa shughuli za kawaida kutapunguzwa na watu wasiokuwa na visa vikali vya maambukizi wanaweza kujitenga majumbani badala ya vituo vya pamoja vya serikali.

Aidha watu hawatahitajika kuonyesha kibali maalum cha afya kwenye simu zao wakati wanapoingia kwenye majengo na maeneo ya umma, isipokuwa tu katika makaazi ya wazee na watoto, hospitali, na shuleni. Sheria hizo mpya pia zimefuta karantini za lazima kwa watu wasiokuwa na dalili za corona.

Hasira dhidi ya sera ya China ya kupambana na Covid ambayo inahusisha kusitishwa kwa shughuli za kawaida, kupimwa kwa mara kwa mara na karantini hata kwa watu wasioambukizwa kulisababisha vurugu ambazo hazijawahi kushuhudiwa tangu maandamano ya mwaka wa 1989 ya kuunga mkono demokrasia.

Chanzo DW






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags