Chelsea kuuza wachezaji ili kumsajili Osimhen

Chelsea kuuza wachezaji ili kumsajili Osimhen

Imeripotiwa kuwa ‘klabu’ ya Chelsea ina mpango wa kupiga bei mastaa wake kadhaa ili kupata Euro 200 milioni ambazo itazitumia kwenye usajili wa ‘straika’ wa Napoli, Victor Osimhen.

Kwa madirisha kadhaa ya usajili, ‘straika’ huyo wa kimataifa wa Nigeria amekuwa akihusishwa na miamba hiyo ya Stamford Bridge, mahali ambako panatajwa hata yeye mwenyewe kupawekea kipaumbele endapo ataamua kuhamia kwenye Ligi Kuu England.

Ripoti zinafichua kwamba baadhi ya wachezaji ambao wanaweza kupigwa bei ni Conor Gallagher, Trevoh Chalobah, Armando Broja, Marc Cucurella, Thiago Silva, Malang Sarr, Kepa Arrizabalaga, Romelu Lukaku na Hakim Ziyech.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags